Nimekuwa bubu nimepigwa na butwa
Mdomo mzito kinywa kama ndondocha
Macho yana magugu sioni mbele najikwa ah
Yani ujanja sina nimezorota
Naona! Joto si joto baridi si baridi
Mwili wa nchoma choma
Naona! Kichwa kinawaka moto
Moyo unakwenda speed
Yani homa si homa, eh!
Vipimo nimemaliza kwa manguri daktari
Waganga matabibu, he he-eh!
Kumbe najilimbikiza maumivu makali
Naongeza maswahibu, oh-oh-oh!
Nimezunguka kote buza na yombo dovya
Sijaaambulia chochote zaidi ya kuchovya chovya
Rudi tuishi sote ujinga tu uliniponza
Jaribu kusahau yote mtima uje kuupoza
Baby, fanya!
Turudiane turudiane tena
Turudiane tuwe kama zamani
Turudiane (fanya turudiane)
Turudiane (turudiane) unirudie baby
Turudiane (oh-oh) tuwe kama zamani
Turudiane
Yalopita yamepita si ndwele
Rudi tugange yajayo we nimekuzoea
Tufanye yamekwisha uje tujenge ya mbele
Yale tuachane nayo mwenzako najidodea
Rudi tufunike kombe mwanaharamu apite
Tusijali tutaonekanaje kwa ndugu jamaa
Nimekubali kwako kibonde acha tu nidhalilike
Sina habari ata wakisemaje nnachotaka furaha
Yale matusi kejeli, vijembe, mafumbo kutupiana
Yote tufanye yaishe, eh-eh-eh!
Najua twapendana kweli sasa ya nini tunazozana
Rudi penzi tudumishee, oh-oh-oh-oh!
Nimezunguka kote buza na yombo dovya (nimezunguruka kote)
Sijaaambulia chochote zaidi ya kuchovya chovya (oh-oh, oh-oh!)
Rudi tuishi sote ujinga tu uliniponza
Jaribu kusahau yote mtima uje kuupoza
Baby fanya!
Turudiane turudiane tena
Turudiane tena, unirudie
Tuwe kama zamani (iyeeh!)
Fanya turudiane (turudiane)
Turudiane tena (unirudie baby)
Turudiane tuwe kama zamani
Turudiane